Tundu Lissu ameshawasili nchini (+picha)
Makamu
Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amewasili nchini na kupokelewa na
viongozi pamoja na mamia ya wafuasi wa chama hicho waliojitokeza katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Lissu anarejea nchini kutokea Ubelgiji alipokwenda kwa ajili ya
matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba
2017.