Baada ya kufukuzwa na Arsenal hatimae Unai Emery apata timu
Unai Emery ,48, anajiunga na Villarreal kama mrithi wa kocha Javi Calleja aliyeoondoka timu hiyo licha ya kumaliza msimu akiiacha Villarreal nafasi ya tano katika msimamo wa LaLiga na kupata nafasi ya kucheza Europa League msimu ujao.
Hii ni mara ya kwanza Unai anarudi kufundisha timu toka alipofukuzwa na Arsenal mwezi November 2019 baada ya kudumu kwa miezi 18 pekee, akiwa kajiunga nao May 2018 kurith nafasi ya Arsene Wenger, Unai amewahi kufundisha kwa mafanikio vilabu vya PSG, Sevilla na Valencia
